.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Juni 2017

BAYERN MUNICH IPO KATIKA NAFASI NZURI YA KUMNASA ALEXIS SANCHEZ

Timu ya Bayern Munich ya Ujerumani ipo katika hatua nzuri ya kunasa saini ya mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez iwapo itashindikana kukubaliana mkataba mpya na timu yake.

Sanchez inaaminika kuwa yupo tayari kuhamia kwa wapinzani wa Arsenal katika Ligi Kuu ya Uingereza timu za Manchester City ama Chelsea, lakini Gunners wanataka ahamie katika ligi nyingine.

Bayern Munich inajiandaa kumfanya Sanchez kuwa mchezaji anayelipwa kitita kikubwa ambapo ripoti za Ujerumani zinasema mchezaji huyo anatarajiwa kupewa kitita cha paundi 350,000 kwa wiki.
     Alexis Sanchez kwa sasa yupo katika majukumu ya kimataifa na timu ya taifa ya Chile

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni