.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Juni 2017

CRISTIANO RONALDO AONGOZA KWA KUINGIZA FEDHA NYINGI KULIKO WANAMICHEZO WOTE DUNIANI

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametetea nafasi yake ya kuwa kinara wa wachezaji wanaolipwa fedha zaidi kwa mujibu wa takwimu za mwaka za jarida la Forbes lenye orodha ya wachezaji 100.

Ronaldo, 32, anajiingizia kitita cha dola milioni 93 kwa mwaka na kumfanya mchezaji huyo raia wa Ureno kuongoza wachezaji wenzake kwa mwaka wa pili mfululizo, kwa kujichumia fedha nyingi.

Kabla ya Ronaldo kutwaa nafasi ya kwanza kwa kuingiza fedha nyingi wanamichezo waliokuwa wakishikilia nafasi hiyo ni nyota wa tenesi Tiger Woods na bondia Floyd Mayweather kwa miaka 15 mfululizo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni