.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Juni 2017

KOCHA ANTONIO CONTE AMUAMBIA DIEGO COSTA KUWA HAMUHITAJI TENA

Mshambuliaji nyota wa Chelsea Diego Costa ameambiwa na kocha wake Antonio Conte kuwa hayupo tena kwenye mipango ya klabu hiyo.

Costa mwenye miaka 28 amefunga magoli 20 kati ya michezo 35 ya Ligi Kuu ya Uingereza na kuisaidia Chelsea kutwaa ubingwa, sasa anajiandaa kuondoka Stamford Bridge.

Amesema kuwa Antonio Conte amemtumia ujumbe unaosema Chelsea haina mpango naye na kuongeza kuwa hamtarajii kuwapo katika kikosi chake cha msimu ujao.

Costa mzaliwa wa Brazil aliyechukua uraia wa Hispania amesema uhusiano wake na kocha Conte umekuwa mbaya katika msimu huu.
         Uhusiano baina ya kocha Antonio Conte na Diego Costa haukuwa mzuri msimu huu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni