.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Juni 2017

REAL MADRID YAICHAKAZA JUVENTUS NA KUTWAA UBINGWA WA UEFA

Mshambuliaji nyota duniani Cristiano Ronaldo amefunga magoli mawili wakati Real Madrid ikitetea ubingwa wake wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa staili ya aina yake baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Juventus katika dimba la Cardiff.

Katika mchezo huo alikuwa Ronaldo aliyeanza kuzifumania nyavu katika dakika ya 20 ya mchezo kabla ya baadaye Mario Mandzukic kuisawazishia Juventus kwa kufunga moja ya magoli mazuri ya fainali za michuano hiyo kwa mpira wa tik-taka.

Real Madrid ilionekana kushindwa kuzuilika katika kipindi cha pili na alikuwa Casemiro aliyefunga goli na kuifanya iongoze tena, kabla ya Ronaldo kuongeza goli la tatu kufuatia krosi ya karibu ya goli iliyopigwa na Luka Modric.

Juventus ilizidi kuchanganyikiwa baada ya mchezaji aliyetokea benchi Juan Cuadrado alipotolewa nje baada ya kupatiwa kadi mbili za njano baada ya kulumbana na Sergio Ramos na kisha baadaye Marco Asensio aliyetokea benchi kuifungia Real goli la nne.

Kwa matokeo hayo kocha wa Real Zinedine Zidane na kikosi chake sasa wameshinda Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili mfululizo na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania La Liga tangu aingie madarakani Januari 2016.
Kocha  Zinedine Zidane  akiwa amebeba kombe walilolitwaa kwa mara ya pili mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Wachezaji wa Real Madrid wakimnyanyua juu shujaa wao Cristiano Ronaldo baada ya kuwasaidia kutwaa ubingwa
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akikata kwa mkasi wavu wa goli ambalo walifanikiwa kupachika magoli matatu kati ya manne waliyofunga
Cristiano Ronaldo akipongezwa na mama yake, huku mpenzi wake akiwa kando yake akimuangalia
Rapa maarufu Mmarekani will.i.am akimpongeza Cristiano Ronaldo kwa kutwaa ubingwa wa UEFA
   Cristiano Jr akisalimiana na Sir Alex Ferguson huku baba yake Cristiano Ronaldo akiangalia

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni