.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 30 Julai 2017

JON JONES ATWAA TENA UBINGWA WA UFC KWA KO

Jon Jones ametwaa tena ubingwa wa UFC wa uzito wa light heavyweight baada ya kurejea tena ulingoni tangu kupita mwaka mmoja, kwa kumdunda kwa KO mpinzani wake Daniel Cormier katika raundi ya tatu.

Pambano lao hilo la marudio baada ya kupita miaka miwili na nusu tangu wakutane kwa mara ya kwanza, lilichezwa kwenye ukumbi wa Honda Center, huko Anaheim, baada ya Jones kuchonga kuwa yeye ni bingwa wa mabingwa katika historia ya mchezo wa UFC.

Katika raundi mbili za kwanza mabondia hao walionyesha ushindani wa nguvu na mchezo mzuri wakipambana bila ya kushikana mara kwa mara, lakini Jones alitumia vyema teke alilompiga Cormier raundi ya tatu kisha kumshambulia vilivyo na kumaliza pambano.
                  Jon Jones akimpiga teke Daniel Cormier lililochangia kumaliza nguvu
             Jon Jones akimshindilia ngumi mfululizo Daniel Cormier na kumaliza kabisa
                 Daniel Cormier akibubujikwa na machozi wakati akihojiwa baada ya kudundwa 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni