.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 30 Julai 2017

REAL MADRID YALALA KATIKA MCHEZO WA EL CLASICO MAREKANI

Gerard Pique amefunga goli la ushindi wakati Neymar akisaidia kupatikana kwa magoli mawili katika mchezo wa El Clasico uliopigwa Marekani ambao Real Madrid ililala kwa magoli 3-2.

Katika mchezo huo ambao refa alilazimika kutoa kadi nne za njano, Lionel Messi alikuwa wakanza kupachika goli wavuni katika dakika tatu tu za mchezo uliochezwa kwenye dimba la Hard Rock.

Kikosi hicho cha Ernesto Valverde kiliongeza goli la pili dakika nne baadaye pale Ivan Rakitic alipounganisha wavuni pasi ya Neymar, kisha baadaye Mateo Kovacic akachomoa goli moja.

Marco Asensio aliipatia Real Madrid goli la pili dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili kwa kuachia shuti lililomshinda kipa Jasper Cillessen, hata hivyo Gerard Pique aliipatua Barcelona goli la ushindi kupitia krosi ya Neymar. 
   Lionel Messi akiangalia mpira alioupiga ukienda kujaa wavuni na kuandika goli la kwanza
                   Mchezaji Ivan Rakitic akifunga goli la pili la Barcelona kwa shuti kali
    Marco Asensio akimpiga chenga beki Jordi Alba na kisha kufunga goli la pili la Real Madrid
      Gerard Pique akiunganisha krosi ya Neymar na kufunga goli la tatu lililoipa ushindi Barcelona

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni