.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 7 Agosti 2017

ARSENAL YAANZA MSIMU MPYA KWA KUTWAA NGAO YA JAMII

Arsenal imetwaa ngao ya jamii baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 kwa mikwaju ya penati, kufuatia kumaliza dakika 90 zikiwa na matokeo ya goli 1-1 dhidi ya Chelsea.

Katika mchezo huo ulioshuhudia Pedro akipewa kadi nyekundu dakika 10 kabla ya mchezo kuisha Chelsea walipata goli la kwanza kupitia Victor Moses na Sead Kolasinac alisawazisha kwa kichwa.

Katika mikwaju ya penati kipa Thibaut Courtois alipaisha juu penati aliyoipiga huku mchezaji mpya Alvaro Morata aliyesajiliwa kwa paundi milioni 55 naye akikosa penati.

Olivier Giroud alifunga penati ya ushindi na kuifanya Arsenal inayonolewa na Arsene Wenger kuanza msimu mpya kwa kutwaa ngao ya jamii.
                                        Victor Moses akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
                      Sead Kolasinac akiruga juu kupiga kwa kichwa mpira uliosawazisha goli 
                                   Mchezaji wa Chelsea Pedro akipewa kadi nyekundu na refa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni