.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 8 Agosti 2017

BALOZI IDDI AKAGUA HUDUMA ZA AFYA WANAZOPATA WANANCHI MKOANI PEMBA

Daktari Mkuu wa Hospitali ya Abdullah Mzee Dr. Haji Mwita Haji Kulia akimtembeza sehemu mbali mbali za Hospitali hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kukagua huduma za afya wanazopatiwa Wananchi mbali mbali Hospitalini hapo.
Mkuu wa Kitengo cha X Ray katika Hospitali ya Rufaa ya Abdullah Mzee iliyopo Mkoani Pemba Dr. Muhsin Aley Ali Kulia Kimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kukagua huduma za uchunguzi wa Afya Hospitalini hapo, wa kwanza kutoka Kushoto ni Daktari Mkuu wa Hospitali ya Abdullah Mzee Dr. Haji Mwita Haji.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishiriki shughuli za uhamasishaji wa uchumaji wa Zao la Karafuu katika Mbiji Changaweni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
Mhandisi Muelekezi wa Kampuni inayosimamia ujenzi wa Ofisi Tatu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mtaa wa Gombani Chake chake Pemba Bwana Mbarouk Juma Mbarouk akimpatia maelezo Balozi Seif aliyefika kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Ofisi hiyo.
Mhandisi Mbarouk akimkaguza Balozi Seif katika maendo mbali mbali ya ndani ya majengo yanayoendelea kujengwa hapo Gombani yatakayozijumuisha Wizara Tatu za Fedha, Katiba na inayosimamia Wanawake na Watoto. Picha na OMPR- ZNZ.

Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuchukuwa hatua za kisheria kwa kutaifisha Karafuu zinazotoroshwa Nchini sambamba na kukichoma moto mara moja chombo kitakachohusika kutaka kusafirisha zao hilo.

Alisema hatua hiyo ya awali ambayo ni miongoni mwa Mikakati ya Serikali ya kukabiliana na magendo ya Karafuu itafuatiwa na wahusika wa utoroshaji wa zao hilo kushikisha katika vyombo vya sheria kwa kuhusika na uhujumu wa Uchumi wa Taifa.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati wa shughuli za uhamasishaji wa uchumaji wa zao la karafuu karafuu hapo katika Kijiji cha Mbiji Changaweni Wilaya ya Mkoani akimalizia ziara yake ya siku mbili Kisiwani Pemba kukagua shughuli za Maendeleo.


Alisema kwa vile Karafuu bado zinaendelea kuwa ndio mtaji Mkuu wa mapato ya Taifa Serikali kamwe haitovumilia wala kukubali kuona vitendo vya magendo ya Karafuu kutoroshwa nje ya Nchi vinaendelea kwa tamaa za Watu wachache.

Balozi Seif alisema tabia hiyo mbovu ya kutorosha mali ya Taifa haimsaidii mtu bali ni kuikosesha Serikali Mapato jambo ambalo athari yake huonekana pale baadhi ya huduma zinapokosekana kutokana na uhaba wa Mtaji wa Serikali unaotokana na chanzo hicho cha Magendo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza Wananchi hasa Wakulima wajitahidi kuzichuma Karafuu zote zilizozaa katika Msimu wa Mwaka huu na baadae kuziuza katika vituo cha Shirika la Taifa la Biashara { ZSTC

Akitoa Taarifa za maandalizi ya Uchumaji wa zao la Karafuu kwa Msimu wa Mwaka huu wa 2017/2018 kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar, Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Kisiwani Pemba Nd. Abdullah Juma Khamis msimu wa uchumuaji waq zao hilo bado haujachanganya vyema.

Nd. Abdulla alisema uvunaji halisi wa zao hilo uliozinduliwa mnamo Tarehe 24 Julai 2017 unatarajiwa kuchanga vizuri baada ya kukamilika kwa Mwezi Mmoja ujao.

Alisema Shirika la Taifa la Biashara Zanzibarv {ZSTC}limeshajiandaa
kwa mtaji pamoja na vifaa ili Karafuu zote zitakazochumwa ziuzwe
kwenye Shirika hilo kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Nchi.

Afisa Mdhamini huyo Wizaraya Baioshara, Viwanda na Masoko alifahamisha
kwamba ununuzi wa zao la Karafuu umeshaanza tokea Tarehe 17 Julai 2017
na tayari Tani zipatazo 97.3 zimeshanunuliwa zikiwa na thamani ya
Shilingi za Kitanzania Bilioni 1.4.

Nd. Abdullah kupitia shughuli hiyo ya uhamasishaji wa uchumaji wa zao
la Karafuu amewakumbusha na kutoa wito kwa Wakulima wazingatie
uchumaji, uchambuaji pamoja na uanikaji mzuri unaozingatia na kukidhi
viwango vya soko la Kimataifa.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Nd. Hemed Suleiman Abdullah alisema
Mashamba ya Serikali yapatayo 366 yameshakodishwa kwa Wafanyabiashara
mbali mbali na kuiingizia Mapato Serikali Kuu zaidi ya Shilingi
Milioni 66,000,000/-.
Alisema ukodishwaji huo umezingatia zaidi kivuja jasho cha Wakulima
waliojitolea kuyatunza Mashamba ya Serikali kwa kupewa upendeleo wa
ukodishwaji wa Mashamba ya Karafuu kwa kupunguziwa asilimia ya Fedha
wanazokodishwa.
Nd. Hemed alisema changamoto liliopo hivi sasa kwa baadhi ya Mashamba
ya Serikali ambayo yalikuwa yakihodhiwa na baadhi ya Watu kwa muda
mrefu ni kuendelea kutumiwa kwa Nyaraka zilizofuta mara baada ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Mkoani alimueleza Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar kwamba Kamati iliyoundwa na Serikali kuyagundua na
baadaye kuyahakiki Mashamba yote ya Serikali imebaini baadhi ya
mashamba hayo yameshauzwa kienyeji bila ya kufuatwa kwa taratibu.
Alisema Kamati hiyo tayari imeshachukuwa hatua za kuwanyang’anya
Mashamba baadhi ya Watu waliokuwa wamejimilikishwa kinyume na taratibu
hizo na kuyarejesha Serikalini na kuwataka Watu waliouziwa kudai fedha
zao kwa waliowauzia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika ziara yake pia
alikagua maendeleo ya ujenzi wa Majengo ya Wizara Tatu za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar unaoendelea katika Mtaa wa Gombani Chake Chake
Pemba.
Mhandisi Muelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa Majengo hayo kutoka Kampuni
ya Quality Building Contructor Bwana Mbarouk Juma Mbarouk alimueleza
Balozi Seif kwamba ujenzi huo unazingatia umakini mkubwa ili kuepuka
kasoro ndogo ndogo zinazoweza kujitokeza kutokana na mazingira halizi
ya ardhi ya sehemu hiyo.
Bwana Mbarouk alisema Majengo hayo ya ghorofa Tatu Tatu yanazijumuisha
kwa pamoja Wizara ya Ajira, Uwezeshaji Wananchi, Wazee, Vijana
Wanawake na Watoto, Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya
Nchi Ofisi ya Rais, Sheria Katiba, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Alisema Afisi hizo ambazo kila Wizara itakuwa na Ngazi yake
inatarajiwa kuwa na Ofisi 150, kumbi Tatu za Mikutano kwa kila Wizara
pamoja na ule Mkubwa utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia Watu 400 kwa
wakati mmoja.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliridhika na
hatua ya ujenzi wa majengo hayo yanayoonyesha kiwango kinachokubalika
hasa kutokana na Maamuzi ya Kampuni ya ujenzi huo kuamua kufyatua
matofali yake wenyewe ili kuepuka udanganyifu unaoweza kuharibu sifa
ya Kampuni hiyo.
Mapema asubuhi Balozi Seif alikagua Huduma za Afya zinazotolewa
katika Hospitali ya Rufaa ya Abdullah Mzee iliyopo Mkoani na kuridhika
na juhudi kubwa inayochukuliwa na Madaktari na wafanyakazi wa
Hospitali hiyo.
Hata hivyo balozi Seif aliutaka Uongozi wa Wizara ya Afya kuhakikisha
kwamba unazifanyia kazi baadhi ya changamoto zinazoikabili Hospitali
hasa upungufu wa Madaktari Bingwa wa maradhi mbali mbali, ukamilishaji
wa baadhi ya Vifaa pamoja na Haki za Wafanyakazi wake.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni