.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 10 Agosti 2017

BALOZI SEIF AELEKEA CUBA KWA ZIARA YA KIKAZI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akiagana na Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa
alipoondoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
kuelekea Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara maalum.

Meya na Manispaa ya Wilaya ya Magharibi “B” Mstahiki Maabadi Ali
Maulid mwenye suti ya kijivu jivu akimtakia safari njema Balozi Seif
katika ziara yake hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Ndugu Silima Haji
Haji mwenye bashasha akimuaga Balozi Seif Ali Iddi aliyeambatana na
aMkewe Mama Asha Suleiman Iddi katika safari hiyo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka
Zanzibar leo asubuhi kupitia Mjini Dar es salaam kuelekea Nchini
Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum.

Balozi Seif katika ziara hiyo ameondoka akifuatana na Mkewe Mama Asha
Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya wasaidizi wake kikazi.

Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar
Balozi Seif aliagwa na baadhi ya Viongozi, Watendaji wa Serikali
pamoja na Viongozi wa Vyama vya Kisiasa viliopo hapa Nchini.

Ziara ya Balozi Seif Nchini Jamuhuri ya Cuba pamoja na mambo mengine
itajumuisha kutembelea Bunge la Nchi hiyo ambapo pia atapata wasaa wa
kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chombo hicho cha juu cha kutunga
Sheria.

Baadae Ballozi Seif atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Elimu,
Naibu Waziri wa Afya pamja na kuona harakati za uzalishaji wa dawa
katika Kiwanda cha Madawa cha Nchi hiyo sambamba na kufanya mazungumzo
ya Ushirikiano wa pande hizo mbili.

Ziara hiyo ya Balozi Seif imelenga kuendeleza ushirikiano wa muda
mrefu ulipo kati ya Cuba na Zanzibar hasa katika Sekta ya Afya na
Elimu ambazo zimeleta mafungamano ya Nchi hizo rafiki Kihistoria.

Othman Khamis Ame 
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
10/7/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni