.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 7 Agosti 2017

KOCHA ANTONIO CONTE ATETEA UAMUZI WA KUMPA COURTOIS KUPIGA PENATI

Antonio Conte ametetea uamuzi wake wa kumpa nafasi ya kupiga penati kipa Thibaut Courtois katika mchezo wa ngao ya jamii ambao Chelsea ilifungwa na Arsenal kwa mikwaju ya penati.

Uteuzi wa kipa huyo kupiga penati ya pili uliwashangaza wengi katika dimba la Wembley na penati aliyoipiga alipoipaisha aliwaduwaza zaidi watu na kugeuka kituko.

Mara moja wakosoaji walimshutumu kocha Conte kwa uamuzi wake huo, lakini yeye amesisitiza kipa huyo raia wa Ubelgiji amekuwa mipigaji mzuri tu wa penati mazoezini.
               Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois akipaisha nje mpira wa penati alioupiga
              Kipa Thibaut Courtois akiwa anashangaa kwa kuangalia juu baada ya kupaisha penati

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni