.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 6 Agosti 2017

MMAREKANI JUSTIN GATLIN AMTIBULIA REKODI USAIN BOLT

Kimya kikubwa kilitawala mbio za mita 100 wanaume katika fainali za mabingwa wa dunia katika uwanja wa London pale Usain Bolt aliposhindwa kutwaa medali ya dhahabu.

Bolt ambaye hizo ni mbio zake za mwisho kabla ya kustaafu kabisa riadha, alijikutwa akishindwa na Mmarekani Justin Gatlin.

Shamra shamra za kumshangalia Bolt zilitumbukia nyongo, baada ya Mmarekani Gatlin ambaye alinaswa mara mbili kutumia dawa za kututumua misuli kushinda.
Muonekano kwa picha iliyopigwa kutokea juu unavyoonyesha Gatlin akimaliza wa kwanza kabla ya Bolt
Justin Gatlin akipiga magoti kutoa heshima kwa Usain Bolt ambaye atastaafu baada ya michuano hiyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni