.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 10 Agosti 2017

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU KENYA ASHINDA KITI CHA UBUNGE

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 nchini Kenya ambaye ni mgombea binafsi ameshinda kiti cha ubunge wa Igembe Kusini baada ya kutangazwa mshindi leo asubuhi na tume ya uchaguzi.

Mwanafunzi huyo John Paul Mwirigi anayesoma Shahada ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya amepata kura 18, 867 dhidi ya mgombea wa Jubilee, Rufus Miriti aliyepata kura 15, 411.

Mwirigi, ambaye atakuwa mbunge kijana kuliko wote nchini Kenya hakuwa na kampeni za gharama kubwa ambapo alitumia kampeni za kutembea kwa mguu kupitia kila nyumba kabla ya kuungwa mkono na waendesha bodaboda.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni