.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 2 Agosti 2017

NEYMAR APEWA RUHUSA KUSHUGHULIKIA UHAMISHO WAKE

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar amepewa ruhusa kuanza mazungumzo ya uhamisho wake utakaoweka rekodi wa kiasi cha paundi milioni 198 kwenda Paris St-Germain.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, amewaambia wachezaji wenzake katika mazoezi hii leo, kwamba anahitaji kuondoka kwenye klabu hiyo ya Hispania.

Tayari amepewa ruhusa na kocha wa Barcelona Ernesto Valverde kutoendelea na mazoezi ili aweze kushughulikia mustakabali wake wa uhamisho.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni