.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 22 Agosti 2017

RAHEEM STERLING AIOKOA MAN CITY WAKATI WAYNE ROONEY AKIZIDI KUWA MTAMU

Raheem Sterling ameiokoa Manchester City iliyobakia na wachezaji 10 na kuinyima Everton ushindi katika usiku ambao Wayne Rooney alifunga goli lake la 200 la Ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester City walijikuta na kibarua kigumu baada ya Rooney kufunga goli na baada ya Kyle Walker kutolewa nje kwa kadi mbili za njano za haraka ndani ya dakika 44.

Kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola hakikuamini matokeo hayo na kilipambana mnono na kufanikiwa kuepuka kipigo cha pili nyumbani wakiwa chini ya Mhispania huyo.
   Mpira uliopigwa na Wayne Rooney ukiwa umempita tobo kipa wa Manchester City na kuandika goli 
   Raheem Sterling akiachia shuti na kuisawazishia Manchester City goli na kufanya matokeo kuwa 1-1

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni