.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 1 Agosti 2017

WAZIRI MKUU ATEMBELA KIWANDA CHA PEPSI NA MABO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Ltd kinachotengeneza vinywaji baridi pamoja na kiwanda cha kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili (mabo) cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, vilivyoko katika eneo la Iyunga Mjini Mbeya.

Amevitembelea viwanda hivyo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa sera ya kujenga uchumi wa viwanda nchini, ambao ndiyo kipaumbe cha Serikali ya Awamu ya Tano. Waziri Mkuu alivitembelea viwanda hivyo jana jioni (Jumatatu, Julai 31, 2017), akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Akiwa katika kiwanda cha Pepsi, Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa kiwanda hicho kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa vinywanji baridi kwenye chupa za plastiki, ambapo amewasihi Watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vya ndani.

Pia Waziri Mkuu aliishauri kampuni hiyo kuendelea kupanua uwekezaji wake hapa nchini kwa kuwa Tanzania ina sera na mazingira mazuri ya uwekezaji. Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1999 kikiwa na wafanyakazi 75 na kwa sasa kina wafanyakazi 190.

“Nawashauri muendelee kuwekeza Tanzania kwani mbali na utulivu wa kisiasa pia sera na mazingira yake ya uwekezaji ni mazuri.”

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi kampuni SBC Tanzania Ltd. Bw. Atif Dar alisema kiwanda cha Mbeya ni cha pili kwa ukubwa wa mauzo ya vinywaji baridi vinavyotengenezwa na kampuni hiyo kikitanguliwa na kiwanda cha mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kwa sasa wanachukua soda zilizofungwa katika chupa za plastiki kutoka katika kiwanda chao cha Dar es Salaam, ambapo waliamua kupanua kiwanda hicho ili waanze kutengeneza soda zilizofungwa katika chupa za plastiki mkoani Mbeya baada ya mahitaji kuongezeka.

Bw. Dar alisema gharama za uwekezaji huo ni dola za Marekani milioni 3.5, ambapo mradi huo unatarajiwa kuanza rasmi Novemba 2017 ambapo mbali na kuuza katika soko la mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pia watasafirisha katika nchi za Zambia na Malawi.

Pia Bw. Dar alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mchangamo wa kiwanda hicho katika uboreshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii.

Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd

Waziri Mkuu alisema mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo vitakavyowawezesha wananchi tununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.

Pia aliwataka Watanzania wote hususani mashirika, taasisi, asasi na mamlaka za Serikali kujenga utamaduni wa kupenda kununua na kutumia na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vilivyopo hapa nchini ili viweze kuimarika na kusaidia kutatua tatizo la ajira.

Alitoa kauli hiyo badaa ya kutembelea kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili (mabo) cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, kilichoko katika eneo la Iyunga Mjini Mbeya. Kiwanda hicho kinatumia malighafi za hapa nchini.

Waziri Mkuu alisema mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo vitakavyowawezesha wananchi kununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMANNE, AGOSTI 1, 2017

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni