.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 19 Septemba 2017

KONGAMANO LA KWANZA LA KITAIFA LA USAFIRI WA ANGA

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka leo akifuatilia mada kwenye Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, linalofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye tai nyekundu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Usafiri wa Anga linalofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kushoto kwa Waziri ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Bw. Hamza Johari.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (mbele) leo akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi (hayupo pichani) aliyekuwa akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, lililoanza leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni