.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 20 Septemba 2017

KONGAMANO LA KWANZA LA KITAIFA LA USAFIRI WA ANGA

Wabunge wa zamani wa majimbo ya Nachingwea na Lilundi, Mhe. Maokola Majogo (kulia) na Anna Abdallah wakipata maelezo mbalimbali ya Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, kutoka kwa Mhandisi Kedrick Chawe na Bi. Harieth Nyalusi katika maonesho yanayokwenda sambamba na Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, lililomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Bw. Geoffrey Tupper (kulia) akikusanya makabrasha mbalimbali yanayotoa maelezo ya viwanja vya ndege kutoka katika meza ya maonesho ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yaliyokuwa yakienda sambamba na Kongamano Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, lililomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bi. Fatma Matimba na Mhandisi Kedrick Chawe wa TAA.
Mhandisi Kedrick Chawe akimfafanulia masuala mbalimbali ya Viwanja vya ndege, Bi. Mwamini Mohamed aliyetaka kujua ujenzi wa jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), wakati wa Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga lililomalizika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka akichangia mada kwenye Kongamano la siku mbili la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, lililomalizika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni