.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 23 Septemba 2017

LUKAKU AISAIDIA MANCHESTER UNITED KUIBUKA NA USHINDI FINYU

Mshambuliaji Romelu Lukaku amefunga goli lake la sita katika Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu huu na kuipatia Manchester United ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Southampton.

Lukaku alitikisa nyavu katika dakika 20 ya mchezo kwa mpira uliogonga mwamba na kurudi baada ya kipa Fraser Forster kupangua mpira wa kichwa wa krosi ya Ashley Young.

Kwa matokeo hayo Manchester United wanaendelea na rekodi ya kutofungwa katika msimu huu na wapo nyuma ya vinara Manchester City kwa tofauti ya magoli.
  Mshambuliaji Romelu Lukaku akifunga goli pekee la Manchester United katika mchezo huo
Southampton walijaribu bila ya mafanikio kurejesha goli hilo ila kipa wa Manchester United alikuwa makini

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni