.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 22 Septemba 2017

SPIKA JOB NDUGAI AUDHURIA MAZISHI YA FAMILIA YA ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA

IMGL6486
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimfariji Mbunge Mstaafu wa Mpwapwa Mjini Mhe. Gregory George Teu (kushoto) kwa Msiba wa familia yake uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, kabla ya kuanza kwa mazishi yatafanyika leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
IMGL6459
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akiwasili katika Msiba wa familia ya Mbunge Mstaafu wa Mpwapwa Mjini Mhe. Gregory George Teu uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, ambapo mazishi yatafanyika mapema leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
IMGL6649
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza viongozi Mbali mbali wa serikali katika kuaga miili ya familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, katika msiba uliofanyika leo nyumbani kwake Mpwapwa Mkoani Dodoma.
IMGL6625
Wananchi Mbali mbali waliohudhuria katika Msiba wa familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, katika mazishi yaliyofanyika leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.

IMGL6835
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akiongoza viongozi Mbali mbali wa serikali katika misa ya kuaga miili ya familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, uliofanyika leo katika kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa)iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
IMGL7248
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiweka Shada ya maua katika mazishi ya familia ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, yaliyofanyika leo katka makaburi ya kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa) iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.

                                                                                           PICHA NA OFISI YA BUNGE

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni