.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 22 Oktoba 2017

HARRY KANE AIONGOZA SPURS KUIFANYIKA KITUMBAYA LIVERPOOL

Magoli mawili ya Harry Kane yameichochea Tottenham kuiadhibu Liverpool yenye beki uchochoro katika dimba la Wembley kwa kuichapa magoli 4-1 na kufikisha pointi sawa na Manchester United katika nafasi ya pili.

Kane alifunga goli la kwanza baada ya dakika nne tu baada ya pasi ya kubetua ya Kieran Trippier kupita juu ya kichwa cha Dejan Lovren, na kumkuta mshambuliaji huyo wa Uingereza aliyetumbukiza mpira kimiani.

Dakika nane baadaye Spurs wakaongeza kupitia kwa Son Heung-min, lakini baadaye Liverpool wakachomoa goli moja kupitia kwa Mohamed Salah. Dele Alli aliongeza goli la tatu na kisha baadaye Kane akafunga goli la nne.
             Harry Kane akifunga goli la kwanza la Spurs kati ya mawili aliyoyafunga
                       Dele Alli akiifungia Tottenham Spurs goli la tatu katika mchezo huo 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni