.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Novemba 2017

PARIS ST-GERMAIN YAIFANYIA UNYAMA WA MWAKA CELTIC

Timu ya Celtic imejikuta ikijuta kuifahamu Paris St-Germain, baada ya kuchakazwa magoli 7-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika dimba la Parc de Princes.

Kikosi cha Brendan Rodgers kilikuwa cha kwanza kufunga goli katika dakika ya kwanza kupitia kwa Moussa Dembele, lakini goli hilo ilikuwa kama wamechokoza nyuki kwenye mzinga.

Neymar alifunga mara mbili na kutengeneza la tatu lililofungwa na Edinson Cavani, na kisha Kylian Mbappe kufunga kabla ya mapumziko.

Marco Verratti, Cavani na Dani Alves walifunga magoli ndani ya dakika tano katika kipindi cha pili na kukifanya kikosi hicho cha Rodgers kupata kipigo cha magoli 7 kwa mara ya kwanza.
                                         Mshambuliaji nyota Mbrazil Neymar akiifungia PSG goli
                             Mfaransa Kylian Mbappe akiwa amepiga mpira uliotinga wavuni

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni