Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
amesema Benki ya Dunia imeahidi kutoa dola bilioni 2.1 ili kusaidia
kujenga eneo la kaskazini-mashariki mwa Nigeria lililosambaratishwa
na machafuko ya miaka kadhaa ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Rais Buhari ametoa kauli hiyo
alipokuwa akiongea Jijini Washington baada ya mazungumzo na maafisa
wa Benki ya Dunia.
Amesema kuwa kipaumbele kinapaswa
kuwekwa katika kujenga upya miundombinu na kuwasaidia wale
waliojikuta wakikimbia makazi yao kutokana na machafuko.
Rais Buhari ameahidi kulidhibiti
kundi la Boko Haram ambalo limeuwa maelfu ya watu nchini Nigeria
tangu mwaka 2009.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni