Chama cha Wananchi Cuf kimesema hakijajitoa katika Ukawa, na kusisitiza kuwa wao bado wapo katika muungano huo unajumuisha vyama vya Chadema, Cuf, Nccr Mageuzi na Nld.
Akitoa taarifa hiyo hivi punde, Naibu Katibu Mkuu wa Cuf Tanzania Bara, Mh Magdalena Sakaya amesema kutokuwepo katika mkutano wa jana wa Ukawa uliokuwa na lengo la kumpata mgombea Urais wa umoja huo, ni kutokana na kuwa na kikao chao ili kuweka mambo sawa nasio kwamba wamejitoa katika umoja huo.
Kumekuwa na tetesi za muungano huo kusambaratika kufuatia mvutano wa nani anafaa kupitishwa kuwa mgombea Urais wa umoja huo kati ya Katibu mkuu wa Chadema, Mh Wilbroad Slaa au Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Lipumba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni