Licha ya kujiorodhesha kufilisika
rapa 50 Cent bado anajikakamua kuonyesha jeuri ya pesa baada ya
kuonekana katika klabu moja ya wasichana wanaocheza nusu utupu huku
akimwaga dola.
Katika video yake iliyotolewa na
chombo kimoja cha Marekani rapa huyo ambaye jina lake halisi ni
Curtis Jackson, anaonekana akiwangalia wasichana hao huku akiwa na
rundo la dola mkononi.
Wasichana hao walionekana wakicheza
kwa kujituma huku rapa 50 Cent akiwarushia dola katika klabu hiyo ya
Ace Of Diamonds iliyopo magharibi mwa Hollywood.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni