Mashabiki wanne wa Chelsea waliogoma
kumruhusu mtu mweusi kuingia katika usafiri wa treni ya aridhini wa
Metro Jijini Paris wamefungiwa kuhudhuria mechi kwa muda unaofikia
hadi miaka mitano
Mashabiki hao Richard Barklie,
kutoka Carrickfergus, Northern Ireland, Joshua Parsons na William
Simpson, wote kutoka Surrey, wamefungiwa kuangalia mechi kwa muda wa
miaka mitano na mahakama ya hakim Magistrates.
Shabiki wengine Jordan Munday,
kutoka Sidcup huko Kent, amefungiwa kwa muda wa miaka mitatu.
Mahakama imewaamuru wasihudhurie mechi za nyumbani amana ugenini kwa
muda wote huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni