Wagombea ubunge wa jimbo la Tabora mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh Aden Rage na Bandora Mirambo hii leo walikutana uso kwa uso walipofika ofisi za CCM wilaya kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge wa Tabora mjini.
Wote wawili katika kuonesha siasa si chuki wala ugomvi walilakiana na kusalimiana kwa uzuri kabisa.
Mh Aden Rage ndiye mbunge aliyemaliza muda wa ubunge wa
Tabora mjiini ambapo alishinda ubunge huo mwaka 2010 kwa kumuangusha kwenye kura za maoni ndani ya CCM
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2005
marehemu Siraju Kaboyonga ambaye naye alimshinda Henry Mgombe mwaka 2005 aliyekuwa mbunge mwaka 2000
.
Hali hii
imeonesha kuwa wapiga kura wa Tabora wamekuwa na tabia ya kutorudisha
mbunge katika kiti hicho kwa mara ya pili
mfululizo, Mh Rage ambaye alipata kuwa mwenyekiti
klabu cha Simba cha jijini Dar bila
shaka atakuwa na kibarua kigumu cha kuuvunja mwiko
huo.
Bandora Mirambo ni mkurugenzi wa kampuni
ya ulinzi ya Salu yenye makao yake
makuu mjini Shinyanga na matawi kadhaa mikoa ya kanda ya
ziwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni