Polisi nchini China wamelazimika kuingia kazini kukabiliana na kundi la vijana watatu Wamarekani, wenye wazimu wa kujiselfisha kwenye minara miyembamba ya majengo marefu duniani.
Polisi hao wamelazimika kuingia kazini kutokana na vijana hao wanaopenda michezo ya hatari kuonekana kuwazidi mbinu walinzi wa kawaida wa majengo hayo na mifumo ya kamera za ulinzi.
Hilo limefuatia picha kadhaa za instagramu zilizowekwa na vijana hao wakiwa wamejiselfisha kwenye mnara mwembamba zaidi duniani ulio juu ya jengo la pili kwa urefu duniani, katika mji wa Shenzhen katika jimbo la Guangdong.
Kabla ya kupanda mnara huo wa hatari, vijana hao wazungu walishawahi kupanda kwenye mnara wa jengo refu zaidi duniani liitwalo Dubai Princess Tower, lenye ghorofa 101, lililopo mji wa Marina, huko Dubai.
Kilichowakera zaidi polisi wa China, ni kuwa mbali hatari ya ya kupanda juu ya minara hiyo, vijana hao pia wanamchezo wa kukaa kwenye kingo za majengo hayo au kingo za vyuma vya minara hiyo ili wajiselfishe kwa picha kali zaidi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni