Mkuu wa genge hatari la dawa za kulevya
Joaquin "El Chapo" Guzman amesafirishwa kwenda Marekani
akitokea Mexico.
Guzman ambaye ni kiongozi hatari wa
genge la Sinaloa amewasili Jijini New York kwa ndege akitokea Ciudad
Juarez.
Guzman, anakabiliwa na adhabu ya
kifungo cha maisha nchini Marekani, iwapo atatiwa hatiani kwa
makosa ya usafirishaji kiwango kikubwa cha dawa za kulevya na kutakatisha
fedha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni