Cristiano Ronaldo amekuwa na wakati
mgumu mno katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
kukabiliwa na ukame wa kutofunga magoli kwa muda wa dakika 523.
Mchezaji huyo bora wa dunia amefunga
magoli mawili tu katika michuano hiyo ya sasa, katika mchezo wa
makundi dhidi ya Sporting Lisbon na Borussia Dortmund.
Ronaldo alishindwa kufunga jana
wakati Madrid ikishinda magoli 3-1 dhidi ya Napoli katika mchezo wa
kwanza wa hatua ya 16 bora.
Cristiano Ronaldo akiwa chini akijaribu kumshawishi refa kuwa kachezewa rafu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni