Bondia Floyd Mayweather ameweka
kando vita yake ya maneno na nyota wa UFC Conor McGregor na kwenda
kuuangalia mchezo wa kikapu wa Los Angeles Clippers na Atlanta Hawks
akiwa na mwanamuziki Mariah Carey.
Wakati hatma ya nyota huyo wa ngumi
aliyestaafu kurejea tena ulingoni ikiwa bado haijulika, jana alienda
kushuhudia mchezo huo wa Ligi ya NBA, kushuhudia Clippers ikiifunga
Hawks pointi 99-84 Jijini Los Angeles.
Mariah Carey akiongea huku akiwa amenyanyua mkono akiwa na Floyd Mayweather
Bondia Floyd Mayweather akiongea na mchezaji wa Atlanta Hawks, Dwight Howard
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni