KONGAMANO LA WANASAYANSI WATAFITI LAMALIZIKA JIJINI MWANZA
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi),
Dkt Leonard Chamuriho (kushoto) akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki wakishiriki Kongamano la
Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria
lililomalizika jana jijini Mwanza.
Bi.
Joyce Kasebela akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa
Baraza la Mawaziri wa Bonde la Ziwa Victoria, ambaye pia ni Waziri wa
Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge baada ya Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwa mmoja wa wadhamini wa Kongamano
la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria
lilimalizika jana jijini Mwanza.
Mwakilishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa Jijini Mwanza, Bi. Dorah Michael (kushoto) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria jana jijini Mwanza.
Bw. Prenanning Pamer mkazi wa Mwanza akipata ufafanuzi wa masuala ya mazingira ndani ya viwanja vya ndege, kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, yaliyomalizika jana jijini Mwanza.
Bi. Joyce Kasebele wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (katikati) akiwa na washiriki wenzake kwenye Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, lililofikia tamati jana jijini Mwanza.
Meneja
wa Kiwanja cha ndege cha Jiji la Mwanza, Bi. Esther Madale (kulia)
akiwa na Bi. Joyce Kasebele wa Kitengo cha Mazingira cha Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali katika Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa
Bonde la Ziwa Victoria. Kongamano hilo lilifanyika Jijini Mwanza.
ASP
Andrew Majaliwa (kulia) akiwa ameshika moja ya vipeperushi vya Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), baada ya kupata maelezo kuhusu
mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki
wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa
Victoria, lililomalizika jana jijini Mwanza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni