Na Dotto Mwaibale
KIKOSI cha Timu ya Ngaya kutoka nchini Comoro kimewasili
nchini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga litakalofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
nchini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga litakalofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imewasili leo saa saba na nusu mchana kwa ndege
ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake.
ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake.
Mara baada ya kuwasili timu hiyo ilipokelewa na wananchi wa nchi hiyo wanaoishi hapa nchini hata hivyo viongozi wa timu hiyo hawakuwa tayari kuzungumza chochote na wanahabari badala yake walipiga picha ya pamoja na wachezaji na kisha kupanda kwenye magari na kuondoka.
Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini humo Yangailiibuka kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo.Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema maandalizi yamchezo huo yamekamilika na kuwa waamuzi wake wanatarajiwa kufika kesho.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni