Zlatan Ibrahimovic amefunga magoli
matatu yaani hat-trick wakati Manchester United ikianza vyema hatua
ya 32 bora katika ligi ya Uropa na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0
dhidi Saint-Etienne.
Ibrahimovic alifunga goli la kwanza
kwa shuti la mpira wa adhabu uliogongwa na kumpoteza muelekeo kipa
Stephane Ruffier, akafunga kiulaini tena mpira wa krosi ya Marcus
Rashford, na kisha baadaye kupata penati ambayo nayo aliitumbukiza
kimiani.
Mchezo huo ulitazamwa na Mama yake
Pogba, Yeo na kaka yake Mathias ambao kama familia walikuwa
wakishuhudia Pogba na kaka yake Florentin anayechezea Saint-Etienne
wakichuana katika mchezo huo.
Mpira uliopigwa na Zlatan Ibrahimovic ukielekea wavuni na kuandika goli la kwanza
Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic wakiangalia mpira wa kichwa uliopigwa na Pogba ukigonga mwamba
Paul Pogba akiongea na na kaka yake Florentin huku akizuia mdomo wake kwa mkono ili asiweze kutambulika anachomuambia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni