Timu ya Chelsea imekabidhiwa kombe
lao la Ligi Kuu ya Uingereza huku ikimaliza ligi kwa ushindi mnono wa
magoli 5-1 dhidi ya timu ya Sunderland inayoshuka daraja, katika
mchezo ambao pia kapteni John Terry aliagwa rasmi.
Katika mchezo huo Chelsea walijikuta
wakifungwa goli la mapema na Javier Manguillo lakini walizinduka
haraka na kusawazisha kupitia kwa Mbrazil Willian, kabla ya baadaye
Eden Hazard kuongeza la pili.
Pedro aliyeingia kuchukua nafasi ya
Hazard alifunga goli tatu kupitia kosa la mpira wa kichwa wa
kurudishwa nyuma uliopigwa na Joleon Lescott huku mchezaji mwingine
aliyetokea benchi Michy Batshuayi kufunga magoli mawili.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte alijikuta akimwagiwa maji ikiwa ni sehemu ya furaha ya ushindi
Kocha Muitaliano Antonio Conte akibusu kombe la Ligi Kuu ya Uingereza waliolitwaa
Mshambuliaji nyota Diego Costa ambaye hatma yake ya kubakia Chelsea ipo mashakana akiwa akiwa amebeba kombe
Nohodha John Terry aliyestaafu soka rasmi akitoa shukurani na neno lake la mwisho kwa mashabiki baada ya kuichezea Chelsea kwa miaka 22
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni