.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 22 Novemba 2017

SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WAFANYABIASHARA WA MBOLEA WANAOKWEPA BEI ELEKEZI

Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza katika Mkutano wa Makatibu Tawala na Washauri wa kilimo wa Mkoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Katika KUKUMBI WA kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya Nov 21 ,2017.

Na EmanuelMadafa,Mbeya

SERIKALI imewataka wafanyabiashara wa mbolea nchini kuhakikisha wanafuata bei elekezi ya uuzaji wa mbolea iliyowekwa na serikali ili kumsaidia mfanyabiashara mdogo aweze kuuza kwa rejareja.

Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Naibu waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa wakati akifungua mkutano wamakatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini .

Amesema kuwa endapo itagundulika kwamba kuna mfanyabiashara wa jumla anamuuzia mfanyabiashara wa rejareja kwa bei itakayomfanya ashindwe kuuza kwa bei elekezi wizara itamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungia biashara yake

Mwanjelwa amesema ofisi yake inaushahidi kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wa jumla wamekuwa wakiwauzia mawakala wanaouza kwa bei elekezi ya serikali hivyo kuleta mkanganyiko na kuwafanya wauze mbolea hiyo kwa bei zaidi ya elekezi .

Amesema katika Mikoa ya Ruvuma,Lindi ,Mtwara ,Mwanza na Geita wapo wafanyabiashara ambao sio waaminifu wamekuwa wakifungua mifuko na kuuza mbolea ya kupandia (DAP) kwa Shilingi 2,000 kwa kilo kwa lengo la kujipatia kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kwa mfuko wa kilo 50 badala ya bei elekezi ya shilingi elfu hamisini na moja.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora wake kwa kufunguliwa kwa kuachwa wazi wafanyabiashara hao wanawaingizia hasara kubwa wakulima hasa katika kipindi cha mavuno.

Kutokana hali hiyo Naibu waziri huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kuacha tabia hiyo mara moja ili kumpa fursa Wakala aweze kuuza kwa bei ya rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao .

Mkutano huo unalenga kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system-BPS )na usimamizi wa mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata mbolea bora kwa bei nafuu sanjali na kuongeza usalishaji wenye tija.

Mwisho.

Washiriki wa Mkutano wa Makatibu Tawala Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini unaolenga kuongeza uwezo uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System -BPS) na Usimamizi wa bei ya mbolea ,katika ukumbu wa mikutano Mkapa jijini Mbeya Nov 21 mwaka huu.

Mshiriki akichangia katika Mkutano huo.......

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa katika Piha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni