Ijumaa, 7 Machi 2014

JOTO LACHOCHEA KUONGEZEKA KWA UGONJWA WA MALARIA DUNIANI


Utafiti umebaini kuwa hali ya hewa ya joto inasababisha kusambaa kwa ugonjwa wa malaria katika maeneo yaliyopo kwenye miinuko.
Watafiti wamebaini kuwa watu wanaoshi kwenye maeneo ya miinuko katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo unaosambazwa na mbu katika majira ya joto.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la madaktari, unaamini kuwa ongezeko la joto duniani litapelekea mamilioni ya watu kuugua ugonjwa wa malaria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni