Jumatatu, 10 Machi 2014

KENYA KUHARIBU MAGARI CHAKAVU YALIYOINGIZWA KINYEMELA

Zaidi ya magari 2,000 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4 za Kenya yanatarajiwa kuharibiwa nchini humo kutokana na kutengenezwa miaka 8 iliyopita, na kuingizwa kinyume na sheria za Kenya.

Tume ya Maadili na Rushwa imeagiza gari hizo zinazoshikiliwa katika bandari ya Mombasa kupondwa pondwa kwa kuwa inachukulia suala la rushwa katika mipaka ya Kenya kwa umakini mno.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Muno Matemu amesema uchunguzi unaendelea kubaini ni kwa namna gani magari hayo yaliingia Kenya, licha ya taifa hilo kupiga marufuku kuingizwa nchini magari yaliyopita miaka nane tangu yatengenezwe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni