Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akiongea na waandishi wa habari
Timu ya soka ya Arsenal leo wanashuka dimbani ugenini nchini Ujerumani kucheza mchezo wa marudiano na miamba ya ligi kuu Ujerumani, Bayern Munich katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Emirates, Arsenal walikubali kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Bayern kwa mabao yaliyofungwa na Kroos na Muller, hivyo leo wanahitaji miujiza ili kusonga mbele katika michuano hiyo
Kikosi cha Arsenal kikijifua tayari kwa mchezo huo wa leo ligi ya mabingwa Ulaya
Wachezaji wa Bayern Munich wakiwa mazoezini kabla ya kucheza na Arsenal hii leo



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni