Jumanne, 11 Machi 2014

MTAALAM WA TABIA ZA UHALIFU ASEMA KILIO CHA OSCAR PISTORIUS HAKINA MAANA YOYOTE


Mtaalam mmoja wa Tabia za Wahalifu nchini Afrika Kusini amesema kitendo cha kuonyesha hila za huzuni mahakamani Oscar Pistorius si dalili kuwa hana hatia ama anahati au anajutia alichofanya ama hajutii.
Mtaalamu huyo Profesa Anni Hesselink amesema mtu anaweza kulia kwa sababu nyingi baada ya kuua mtu.
Mtaalam huyo ambaye pia aliwahi kuwa hakimu muandamizi,amesema watu hulia kwa kuwa huenda wakafungwa, ama kwa kumkumbuka mtu aliyemuua au kwa kufikiria kuwa maisha yake yote ya badae ameyaharibu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni