Oscar Pistorius ametapika kizimbani hii
leo wakati mtaalam aliyeufanyia uchunguzi mwili wa aliyekuwa mpenzi
wake Reeva Steenkamp akitoa maelezo ya kimichoro yanayoonyesha jinsi
marehemu alivyoumia.
Mwanariadha huyo mlemavu alienda kwenye
ndoo ya taka kutapika wakati Profesa Gert Saayman akitoa maelezo ya
kutisha kuhusiana majeraha kadhaa ya risasi aliyomsababishia mpenzi
wake siku ya tukio hilo.
Profesa Saayman ameiambia mahakama Miss
Steenkamp alipigwa risasi mara nne katika eneo la juu la kulia la
kichwani, kwenye kiwiko cha mkono wa kulia, kwenye paja la kulia na
upande wa mkono wa kushoto.
Wakati ushahidi huo ukitolewa mahakama
ililazimika kuhairisha mara mbili wakati Pistorius alipoangua kilio
huku mabega yake yakitetemeka



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni