Ijumaa, 14 Machi 2014

PICHA ZINAZOMUONYESHA PISTORIUS AKIWA NA MICHIRIZI YA DAMU ZAONYESHWA MAHAKAMANI


Picha za siku Oscar Pistorius alipomua mpenzi wake zimeonyeshwa mahakamani ambapo mwanariadha huyo mlemavu alionekana akiwa kifua wazi huku kaptura aliyoivaa ikiwa imelowa damu na pia miguu yake ya bandia ikiwa na michirizi ya damu.
 

Maafisa polisi wa mwanzo kufika katika tukio hilo walimkuta Pistorius akikimbia kimbia jikoni akiwa kwenye hali ya masikitiko huku damu zilizokuwa zikimchuruzika zikiacha michirizi kwenye nyumba nzima.
Picha hizo ni miongoni mwa picha za kuogofya zilizochukuliwa na polisi baada ya Pistorius kumpiga risasi Reeva Steenkamp, ambapo miongoni mwao ilionyesha mwili wa marehemu na kumfanya Pistorius kutapika kizimbani. 
      Pistorius akiwa amejiinamia mahakamani wakati kesi yake ikiendele hii leo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni