Jumanne, 11 Machi 2014

SHAHIDI ASEMA OSCAR PISTORIUS ANAPENDA MNO SILAHA NA KUFYATUA RISASI


Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius anapenda mno silaha na katika tukio moja alicheka mara baada ya kufyatua risasi juu ya uwazi wa paa la gari, mahakama inayosikiliza kesi yake ya mauaji imeelezwa hii leo.

Mmoja wa marafiki wa mwanariadha huyo mlemavu aitwae Darren Fresco, ameiambia mahakama ya Pretoria kuhusu jinsi Pistorius alivyovyatua risasi hewani mara mbili akiwa nae.
Fresco amesema katika tukio moja alikuwa akiendesha gari akiwa na Pistorius ambapo alitoa bastola yake na kufyatua juu uwazi wa paa la gari bila ya yeye kujua jambo lililomstua na kuyumba wakati akiinama chini na alipomuuliza kama anakichaa Pistorius aliishia kucheka tu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni