Mafisa wa Marekani wanaosaidia kutafuta Ndege ya Malaysia namba MH370, sasa wameelekeza nguvu zao katika eneo la bahari ya Hindi.
Hata hivyo afisa mmoja wa Marekani amesema hatua hiyo haina maana ya kuwa wamepata taarifa kuwa ndege imeanguka katika bahari hiyo.
Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Malaysia ikiwa na abiria 239 ilipotea siku ya Jumamosi, hadi sasa msako wake haujafanikiwa kuipata.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni