Jumatano, 27 Mei 2015

WAZIRI MKUU WA LIBYA ABDULLAH AL-THINNI AMENUSURIKA JARIBIO LA KUUWAWA

Waziri Mkuu wa Libya Abdullah al-Thinni amesema amenusurika jaribio la kuuwawa na watu wenye silaha walioshambulia gari lake katika mji wa Tobruk.

Akiongea na televisheni ya habari ya al-Arabiya al-Thinni amesema anamshukuru Mungu kumuepusha na risasi zilizolenga gari lake wakati akitoka kwenye kikao cha bunge.

Msemaji wa serikali ya Libya amesema waziri mkuu hakupata jeraha lolote katika shambulio hilo ila mmoja wa walinzi wake amejeruhiwa.

Nchi ya Libya imekuwa kwenye machafuko tangu Muammar Gaddafi ang'olewe madarakani mnamo mwaka 2011.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni