Alhamisi, 13 Machi 2014

AIR MALAYSIA IMEANGUKA BAHARINI? CHINA YATOA PICHA ZINAZOONYESHA MABAKI YA KITU KAMA YA NDEGE BAHARINI KUSINI MWA NCHI HIYO

 Picha za satelaiti zilizotolewa na China zimeonyesha kitu kikiwa baharini kama mabaki ya ndege kikielea katika bahari kusini mwa China na kuzidisha hofu kuwa uhenda mabaki hayo yakawa ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea toka ijumaa iliyopita ikiwa na abiria 239 kutoka mataifa 14 ( pichani juu ) japo bado haijathibitishwa na upande wowote.

China ilitoa mitambo yake ipatayo 10 ya Satelaiti kusaidi kuitafuta ndege hiyo inayosadikiwa kuwa imeanguka baharini baada ya kuondoka Kuala Lumpar kuelekea Beijing.

Picha za vifaa hivyo vitatu, ambavyo moja ina upana wa takriban mita 24 kwa 22, zilichukuliwa siku ya Jumapili, siku moja tu baada ya ndege hiyo kupotea, lakini zilichapishwa siku ya Jumatano.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni