Mjini Paris Ufaransa, wenyeji Paris Saint Germain wameutumia vyeam uwanja wao wa nyumbani baada ya kuifunga Bayer Leverkusen waliosafiri kutoka Ujerumani mabao 2-1 katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, matokeo ambayo yameivusha PSG hadi hatua ya robo fainali ya michuano mikubwa kabisa barani Ulaya.
PSG wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 6-1. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Ujerumani, PSG waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0. Mabao ya jana ya Paris St Germain yaliwekwa kimiani Marquinhos kunako dakika ya 13 ya mchezo kabla ya mchezaji Lavezzi kufunga la pili dakika ya 53. Bao la Bayer Leverkusen lilifungwa na Sam dakika ya 6
Mwamuzi wa mchezo huo akimzawadia kadi nyekundu mchezaji wa Leverkusen, Emre Can kadi nyekundu dakika ya 68 katika mchezo huo wa jana usiku



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni