Ijumaa, 7 Machi 2014

'DAUSDEDIT KAHWA' AULA SAFARI YA BRAZILI KUPITIA BIA YA SERENGETI






Akiongea kwa furaha iliyopita kifani kwa njia ya simu mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazil Deusdedit Kahwa kutoka Mbezi, Dares Salaam alisema alipata mshangao mkubwa sana kwa kuwa hakutarajia kupata bahati hii ya kuwa mshindi wa tiketi na alishiriki promosheni hii baada ya kuona matangazo yake kwenye televisheni. 

Aliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa  kumpa fursa hiyo kubwa katika maisha yake na kuipongeza kwa kuwajali wateja wake kwa kuwapa zawadi mbalimali zinogusa maisha yao. “nimefurahi sana na ninajiona mwenye bahati sana kwa kushinda zawadi hii kubwa, hii ni mara ya kwanza kushinda zawadi katika promosheni hii na nimepata zawadi kubwa sana na itakuwa ni mara yangu ya kwanza kutoka nje ya nchi, nawashukuru sana Serengeti kwa kutujali wateja wao” alimalizia Deusdedit

Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo alisema kuwa promosheni hiyo ipo wazi kwa wanywaji wote wa bia ya Serengeti, na mpaka sasa kumekuwa na washindi Zaidi ya 50000 waliojishindia bia za bure na pia zaidi ya washindi 2000 wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 5000 na 10,000. Washindi waliojishindia simu za Samsung tab katika droo ya leo ni Deo Msofe kutoka Kiboroloni, Moshi na Jeremiah Ndelekwa kutoka Arusha. Pia wamepatikana washindi watano (5) wa ving’amuzi ambao wote kwa pamoja watakabidhwa zawadi zao katika sherehe maalum.


Kunywa kistaarabu. Washiriki wanatakiwa kuwa na umri unaozidi miaka 18. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni