Jumapili, 9 Machi 2014

FC BARCELONA YALALA KWA REAL VALLADOLID, YACHAPWA 1-0

Fc Barcelona jana walijikuta wana wakati mgumu katika mbio za ubingwa wa ligi kuu nchni Hispania " La Liga " baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Real Valladolid waliokuwa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani. Bao hilo la Valladolid liliwekwa kimiani na Fausto Rossi.
 Barcelona pamoja na kukchezesha kikosi chake kamili akiwemo Messi, Neymar na wengineo lakini walishindwa kufurukuta mbele ya Valladolid na kuziachia pointi 3 ugenini
Duh!! Pamoja na chenga chenga zangu na mbio mbio zooote lakini leo nimeshindwa kufunga? Ni kama Messi anajiuliza baada ya mchezo kumalizika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni