Rada imeonyesha kuwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia ambayo imepotea kwa zaidi ya saa 24, huende iligeuza safari yake na kurejea ilipotoka.
Timu ya uokoaji imekuwa ikizidisha
jitihada za kutafuta ndege hiyo kwa kuongeza upana wa eneo la zooezi
hilo.
Wachunguzi pia wanaangalia picha za
CCTV zinazoonyesha abiria wawili ambao wanaaminika wamepanda ndege
hiyo kwa kutumia pasi za wizi.
Ndege hiyo MH370 ikitokea Kuala Lumpur
kwenda Beijing ilitoweka angani Kusini mwa Vietnam ikiwa na abiria
239.
Msako wa angani ukiendelea kuitafuta ndege iliyopotea


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni