Jumapili, 9 Machi 2014

SAMUEL ETO'O ASHANGILIA GOLI KWA KUWABEZA WANAODAI YEYE NI KIKONGWE

Ushangialia wa goli wa mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o umekuwa gumzo baada ya hapo jana kupachika bao na kushangilia kama kikongwe huku akishika mti wa kwenye kona kama mkongojo, katika mchezo ambao Chelesea ilishindia 4-0 Tottenham.

Eto'o ambaye amekuwa akilaumiwa kuwa ni kikongwe, ambaye pia hata kocha wake Jose Mourinho alinukuliwa akisema kwa mzaha kuwa Eto'o ni kama mchezaji mwenye umri wa miaka 35, alipachika bao hilo huku akiwa ametimiza umri wa miaka 33 siku ya Jumatatu. 
                                Hapa 'Kikongwe' Eto'o akipachika bao hilo murwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni